TAKUKURU KINONDONI YABAINI MAPUNGUFU KWENYE MIRADI

 


Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni Christian Nyakizee akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2025

...............

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Kinondoni imefuatilia miradi mitano (5) yenye thamani ya zaidi ya Shs. Bill. 202 huku miwili yenye thamani ya zaidi ya Bill. 194 kukutwa na mapungufu ikiwemo kutokamilika kwa wakati kutokana na Ucheleweshwaji wa Fedha kutoka kwenye chanzo na kuchelewa kufika kwenye mradi

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni,Christian Nyakizee ameeleza hayo leo Jijini Dar es Salaam,wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha Januari hadi Marchi 2025 ambapo amesema miradi hiyo ilihusu sekta ya Miundombinu(Barabara),Elimu na Maendeleo ya Jamii.

Aidha Nyakizee amesema katika kipindi hicho TAKUKURU imefanya uchambuzi wa mifumo mbalimbali ili kubaini mianya ya Rushwa katika maeneo ya Kiutendaji ya Ofisi,taasisi au idara mbalimbali na kuidhibhiti huku wakifanya uchambuzi wa mfumo wenye makadirio na makusanyo ya mapato ya Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni.

Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni amesema katika kipindi cha miezi mitatu wamepokea malalamika 120 na kati ya hayo 76 yalihusu Rushwa na 44 hayakuhusu Rushwa ambapo pia wamefungua mashauri mapya sita katika mahakama ya Kinondoni na Mahakama ya Wilaya ya Ubungo na Jamhuri imeshinda shauri moja na kushindwa mashauri mawili huku Mashauri 27 yanaendelea Mahakamani

Hata hivyo,Mkuu huyo wa TAKUKURU Kinondoni amesema kuelekea Uchaguzi Mkuu wataendelea kuelimisha wananchi wajue madhara ya Rushwa na wahamasike kushirikiana na TAKUKURU kutokemeza Rushwa kuanzia sasa hami wakati na baada ya uchaguzi.

 Hata hivyo Taasisi hiyo imeendelea kwasisitiza wananchi kushirikiana na taasisi hiyo ikiwemo kutoa taarifa pindi wanapobaini vitendo vya rushwa katika maeneo yao.









0/Post a Comment/Comments