MFUKO wa Mawasiliano kwa WOte (USCAF) umesema katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya sita shule za umma 469 zimepelekewa vifaa vya TEHAMA lengo likiwa ni kukuza ujuzi wa TEHAMA kwa Wanafunzi na Walimu nchini.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa USCAF Mhandisi Peter Mwasalyanda katika kikao kazi cha wahariri na waandishi wa habari chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo Mhandisi Mwasalyanda amesema jumla ya shule za umma 1,121 zimefikishiwa vifaa vya TEHAMA kwa wastani wa Kompyuta tano, printa moja na Projecta moja.
Kuhusu mafunzo ya TEHAMA kwa walimu Mhandisi Mwasalyanda ameeleza kuwa Lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo walimu kutatua matatizo ya vifaa vya TEHAMA.
Kwamba Walimu 3,798 wamepata mafunzo hayo katika shule 1,791 ambapo kwa Zanzibar ni Walimu 326 na kwa Tanzania Bara Walimu 3,180, mafunzo hutolewa DIT, UDOM na MUST na kwamba katika kipindi cha miaka minne ya Awamu ya Sita Walimu 1,585 Wamepata mafunzo ya TEHAMA.
Mhandisi Mwasalyanda akizungumzia siku ya wasichana na TEHAMA, amesema maadhimisho hayo hufanyika mwezi April kila mwaka na kwamba lengo ni kuhamasisha na kukuza uelewa wa masuala ya TEHAMA kwa wasichana ambapo mpaka kufikia sasa wametoa mafunzo kwa wanafunzi takribani 1,202.
Kwamba Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa mafunzo kwa wanafunzi takribani 490 kutoka shule 304 ambapo Mwaka 2024/2025 Mafunzo yamefanyika Mwezi Aprili kwa wanafunzi wa kike takribani 248 wameshiriki mafunzo haya na yanasaidia na kuhamasisha watoto wakike kupenda masomo ya Sayansi.
Kuhusu vifaa vya TEHAMA kwa shule zenye mahitaji maalumu, Mhandisi Mwasalyanda ameeleza kuwa Shule 22 zitafikishiwa vifaa vya TEHAMA ambapo vifaa hivyo ni pamoja na TV, Braille Machine (Nukta Nundu) Orbit reader (Machine za Kisasa), Laptops, Embosser (Printa ya nukta nundu), Digital voice recorders, Magnifiers.
Post a Comment