Waziri wa Afya Jenista Joakim Mhagama amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amehakikisha anaweka mazingira rafiki kwa mama mjamzito kwa kuhakikisha anaanzisha dharura ya usafiri (M-MAMA) ili mama mjamzito aweze kufika kwenye kituo kikubwa kwa haraka na kuokoa maisha yake.
Amebainisha hayo leo June 9,2025 katika hafla ya upokeaji na kukabidhi vifaa (nepi) za watoto wachanga vilivyotolewa na kampuni ya Doweicare limited katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma . “Uhai wa wakina mama ni uhai wa watanzania wote na ni fanikio la Rais wetu kwa kuhakikisha anafanya yafuatayo, kwa muda mfupi aliasisi huduma ya uhai wa wakina mama kwa kutoa dharura ya usafiri inayojulikana maarufu inayojulikana M-MAMA ili mama apate rufaa kwa udharura wa usafiri na kufika kwenye kituo kikubwa aweze kuokoa maisha yake “ amesema Waziri Mhagama.
Waziri Mhagama Ameongeza kuwa Dkt. Samia alianzisha huduma nyingine ya dharura ambayo ni upasuaji wakati mama anaposhindwa kujifungua apatiwe upasuaji wa dharura.”Alianzisha huduma ya dharura nyingine ya upasuaji pale mama anaposhindwa kujifungua kwa Sababu ya vikwazo na visababishi apatiwe upasuaji wa dharura “ ameongeza Waziri Mhagama
Aidha amesema kuwa wahudumu wa Afya wameongezewa ujuzi kupitia Madaktari bingwa wa Samia iliyoanzishwa kwa lengo la kusaidia huduma za uzazi kwa wakina mama lakini madaktari hao wamesaidia huduma za uzazi na huduma nyingine
Post a Comment