DUCE NA UDSM WAZINDUA MRADI WA STEP EA KWA MABORESHO YA ELIMU AFRIKA MASHARIKI

::::::::


Katika jitihada za kuinua ubora wa elimu nchini, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamezindua rasmi mradi wa STEP EA — Strengthening Teacher Education and Practice in East Africa — mradi ambao utafanyika kwa kipindi cha miezi 18.

Mradi huo una lengo la kuimarisha viwango vya ufundishaji, kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu, na kuimarisha utekelezaji wa sera za elimu zinazohusu mafunzo ya ualimu katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Nelson Boniface alisema kuwa mradi wa STEP EA utawawezesha walimu kufundisha kwa tija zaidi kwa kutumia mbinu shirikishi na bunifu. Aidha, mradi huu unalenga kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili walimu katika mazingira yao ya kazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha DUCE, Profesa Steven Osward, amesema kuwa mafanikio ya mradi huo hayatabaki ndani ya chuo hicho pekee bali yatanufaisha taifa zima kwa ujumla.

Mradi wa STEP EA unatekelezwa kwa ushirikiano wa karibu kati ya DUCE, UDSM na wadau mbalimbali wa elimu, na unatarajiwa kuwa mfano bora wa uboreshaji wa taaluma ya ualimu katika kanda ya Afrika Mashariki.



























0/Post a Comment/Comments