KESI YA LISSU KURUSHWA MUBASHARA ( LIVE)


 ::::::

Mahakama ya Tanzania imesema Shauri la Jinai Namba 8606/2025 na Namba 8607/2025 kati ya Jamhuri na Tundu Lissu, ambayo yamepangwa kutajwa na kusikilizwa Juni 2, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mwenendo wote utarushwa mubashara (live) na pia Mshtakiwa atafikishwa Mahakamani

Taarifa ya Mahakama imeeleza, lengo ni kuwawezesha Wananchi kufuatilia bila kuwa na ulazima wa kufika Mahakamani, pia ni Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania kuimarisha uwazi, uwajibikaji na matumizi ya teknolojia katika huduma ya utoaji haki

Taarifa imeeleza Mahakama ya Wazi Kisutu ni ndogo, inachukua Watu 80, hivyo imekubalika watakaoingia ni Mawakili wa Serikali na Watu wengine (10), Mawakili Utetezi na Watu wengine (60) na Waandishi wa Habari (10).


0/Post a Comment/Comments