WANAFUNZI 214141 WACHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI



::::::


Na Ester Maile  Dodoma 

Jumla ya wanafunzi 214141 ikiwemo wasichana116624

wamechaguliwa kujiunga  kidato cha tano na vyuo vya Elimu ya ufundi ikijumuisha na wanafunzi 1028 wenye uhitaji maalum.

Haya yamebainishwa leo  tarehe  6 June 2025 jijini Dodoma  na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Mohamed Mchengerwa wakati wa mkutano na waandishi wahabari akitoa taarifa kwa umma kuhusu uchanguzi wa wanagunzi wa takaojiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi mwaka 2025.

Aidha Mchengerwa amebainisha kuwa wanafunzi 149818 sawa na asilimia 69.96 wakiwemo wasichana 76491 na wavulana 73327 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule 694 za Sekondary za serikali.

Pia wanafunzi 141146 wakiwemo wasichana 72337 na wavulana 68809 wamepangiwa katika shule za bweni .

Hata hivyo  mhula wa kwanza kwa wanafunzi wa kidato cha tano unatarajia kuanza tarehe 08 julai 2025 hivyo wanafunzi wote waliopangiwa kujiunga na kidato cha tano wanatakiwa kuripoti shuleni kuanzia tarehe 06 julai hadi tarehe  21 julai 2025.




 

0/Post a Comment/Comments