Na Ester Maile Dodoma
Zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya kikao cha uteuzi wa wagombea wa Ubunge na Udiwani wa ChamaCha Mapinduzi (CCM), kufanyika jijini Dodoma Presha inazidi kupanda ndani ya Chama hicho na sasa Mkutano Mkuu Maalum unatarajiwa kufanyika kesho.
Tofauti na mikutano mengine Mkutano Mkuu huo maalumu unatarajiwa kufanyika kwa njia ya mtandao huku ajenda kuu ikitajwa kuwa ni marekebisho madogo ya Katiba.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi na Mafunzo Amos Makala, amesema hayo leo Julai 25, jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mandalizi ya mkutano huo.
Makala amesema kumekuwapo na maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mkutano huo unatarajiwa kufanyika kwa njia ya mtandao.
"Ajenda ya mkutano huu maalum ni moja tuu ambayo ni mabadiliko madogo ya katiba ambayo yawezikufanywa na kilao chochote zaidi ya mkutano mkuu.
"Mabadiliko ya katiba hayawezi kufanywa na NEC, Kamati Kuu wala vikao vya Sekretarieti bali ni wenye katiba yao ambao ni mkutano mkuu," amesisitiza.
Amesema kwa mujibu wa katiba ya chama cha mapinduzi CCM, inawaruhusu kufanya mkutano mkuu maalum kwa njia ya mtandao pale wanapoona inafaa.
Amesema hadi sasa maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na kwa mara ya kwanza watu watakwenda kushuhudi chama hicho kikifanya mkutano mkuu kwa njia ya mtandao.
"Maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100, wilaya zipo tayari mikoa yote ipo tayari Sekretarieti tunaendelea na maandalizi ili kufanikisha mkutano huu mkuu maalum ambao utatanguliwa na vikao vya kamati kuu na halmshauri kuu ya CCM,"amesema
Post a Comment