Na Ester Maile Dodoma
Bilioni 30 zimekusanywa kutoka kwenye shughuli mbalimbali na kuongeza pato katika mkoa wa Singida kwa kipindi cha miaka minne.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego leo 04 julai 2025 katiak ukumbi wa idara habari maelezo jijini Dodoma wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Mkoa huo kwa miaka minne ya serikali ya awamu ya sita.
Dendego Amesema kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Serikali ilitenga kiasi cha shilingi bilion 180.25nakufanikisha kutoka shilingi bilioni 153.80 sawa na asilimia 85 ya bajeti hiyo ambapo mwaka uliofuata wa 2021/2022 ulipata ongezeko ambapo shilingi bilioni 199.42 zilitengwa, na serikali ilitoa shilingi bilion 202.44 ikiwa ni utekelezaji wa asilimia 102.
Post a Comment