ANAYEDAIWA KUMCHOMA MPENZI WAKE NDANI YA NYUMBA AKAMATWA

 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Muliro Jumanne,

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam  linamshikilia Grace Mushi miaka 25 kwa tuhuma za kumchoma moto ndani ya nyumba aliyekuwa mpenzi wake, Khamis Abdallaah miaka 25.

Akizungumza leo Dar es salaam Kamanda wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema kuwa  tukio hilo lilitokea Julai 16 saa nane usiku maeneo ya kwa Mzungu Mbezi Makabe katika Wilaya ya Ubungo.

 Aidha amesema mtuhumiwa aliamka usiku na kumfungia ndani Khamis kisha kumwaga petroli na kuichoma moto nyumba hiyo kitendo kilichosababisha kifo cha mwanaume huyo . 

Kamanda amesema kuwa Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kimapenzi.




0/Post a Comment/Comments