Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinafutilia kwa makini mienendo ya baadhi viongozi wake ambao wamekuwa wakipotosha umma na kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu na maadili ya chama.
Hayo yamesemwa leo Jumatatu Julai 26, 2021 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.
Ameongeza kuwa CCM inawahakikishia wanachama na Watanzania kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote ambao wanatumia nafasi iyo kusukuma ajenda zao binafsi kwa mujibu wa Katiba, kanuni za maadili na uongozi za CCM.

Post a Comment