Wakati umefika sasa wa kusema kwaheri kwa baadhi ya vitu ambavyo vilikua vikwazo kwako wewe mwanafunzi, kwani kampuni yako pendwa ya itel imesikia kilio chako na kuamua kukupa kile ambacho unastahili.
Sasa itel wameamua kuzidisha kusambaza upendo kwa kuwaletea wanafunzi punguzo kabambe wakiwa wananunua laptop zao za Able 1. Ikumbukwe kua hivi karibuni mwanzoni mwa mwezi wa saba itel walizindua bidhaa nyingi mbali na simu, miongoni mwa bidhaa hizo ilikuwepo Laptop yao mpya waliyoipa jina la Able 1.

Zikiwa zimetengenezwa madhubuti kabisa kumlenga mtanzania, Laptop hizi za itel zimejaa sifa ambazo zintosha kabisa katika matumizi ya kila siku kwa mwanafunzi, mfanyakazi au hata matumizi binafsi. Kuanzia kwenye design, operating system, storage, hata na features zingine zote, laptop hii imezingatia ubora wa hali ya juu na teknolojia ya kisasa. Hii inatokana na dhamira ya bidhaa mpya za itel ya kufuata malengo ya kuwapa wateja vifaa bora vinayoenda na wakati.

Kwa wewe mwanafunzi unaweza kufurahia ofa ambayo itel wameiweka kwa mwezi huu wote wa saba. Ili kupata punguzo kabambe fika katika maduka ya little more, itel authorized shops au piga namba 0687830821 kwa maelezo Zaidi.
Post a Comment