Mkuu wa mkoa wa Dar essalaam amewataka LATRA kusimamia Level seat
Aelekeza *Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya* kusimamia Utekelezaji wa *Mwongozo wa Wizara ya Afya*.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amewataka Wananchi kuchukuwa *tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona* ambapo amepiga *marufuku* Wananchi kuingia kwenye *vyombo vya usafiri na sehemu za kutoa huduma pasipo kuvaa barakoa.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo Kufuatia *Mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya* ambapo amesema watafanya *ziara za kustukiza kwenye Vituo vya Daladala, Feri, Stendi, Mabasi ya Mwendokasi, maeneo ya Masoko na sehemu zote za kutoa huduma ili kuangalia Utekelezaji wa agizo hilo.*
Aidha *RC Makalla* amesema *Serikali imejipanga kutoa huduma Bora za matibabu kwa wagonjwa* wote watakaofika hospital na kuwataka *Wananchi watakaoona dalili za Corona kuwahi vituo vya Afya.*
*"TUNAKULINDA NA WEWE UTULINDE, VAA BARAKOA KWA MUSTAKABALI WA AFYA YAKO NA WENGINE*.

Post a Comment