MATUMIZI YA MAKAA YA MAWE HUSAIDIA KUPUNGUZA UKATAJI MITI HOVYO

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Prof. Esnat Chaggu (aliyesimama), akitoa salamu ya utambulisho kwa uongozi wa Mgodi wa Tancoal baada ya kuwasili katika Mgodi huo.






 Mkurugwnzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Mhandisi Dkt.  Samuel Gwamaka (aliyenyanyua mkono), akizungumza jambo kwa Bodi ya Wakurugenzi ya NEMC wakati walipokuwa wakikagua Mgodi.





. Mtaalam wa Miamba Bwa. Matiko Paul akitoa ufafanuzi kwa Bodi ya Wakurugenzi wa NEMC  juu ya namna wanavyofanya shughuli zao katika Mgodi wa Ngaka.





 Sehemu ya Miamba inayotumika kutolea makaa ya mawe katika Mgodi wa Ngaka  uliopo kijiji cha Ruanda Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.





Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Prof. Esnat Chaggu amesema kuwa, matumizi ya makaa ya awe ni nishati mbadala ambayo inasaidia kupunguza matumizi ya mkaa na kuni hivyo kupelekea kupungua kwa kiasi kikubwa ukataji miti. 

Ameyasema hayo alipokuwa katika Mgodi wa makaa ya mawe ya Ngaka uliopo kijiji cha Ruanda Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma, unaomilikiwa na Kampuni ya Tancoal Energy Limited, amesema kuwa makaa ya mawe ni muhimu sana kwa ajili ya nisharti mbadala kama inavyofahamika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani mwaka huu Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesisitiza kutafuta nishati Mbadala kuepuka ukataji miti hovyo.

Aidha Prof Esnat ameeleza kuwa makaa ya mawe yanaweza kutumika katika Taasisi mbalimbali ikiwemo shule, jeshi na hata majumbani kama nishati mbadala kwaajili ya kupikia. 

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NEMC Prof. Hussein Sosovere amesema kuwa, Bodi imetembelea mradi huu kuona shughuli za uchimbaji wa madini kama unazingatia matakwa ya sheria ya mwaka 2004. Amesema kuwa mradi huu unafaida lakini kunachangamoto nyingi za kimazingira kama haujazingatiwa ipasavyo, changamto hizo  ikiwemo uchafuzi katika vyanzo vya maji, kelele na vumbi.

“Hivyo tunawahimiza kampuni hii na NEMC kwa pamoja kushirikiana katika kuhakikisha vyanzo vya maji havichafuliwi ili kuweza kuepusha uchafuzi wa mazingira na afya za binadamu kuwa salama” Prof Sosovere 

Naye Meneja wa NEMC Kanda ya Kusini Bwa.Jamal Baruti amesema kuwa, kila shughuli inayofanywa na binadamu inaathari kwa mazingira hivyo ni jukumu la Baraza na jamii kuhakikisha uwekezaji wowote unafanyika bila ya kuathiri mazingira yetu 

“Sisi kama Baraza ikiwa kama jicho katika kusimamia mazingira tumeweza kutoa ushauri na maelekezo katika suala la udhibiti wa vumbi na maji machafu ya mgodi ambayo yanaweza kusababisha uchafuzi katika vyanzo vya maji. Hivyo nitoe wito kwa makampuni mengine yanayohusika na uchimbaji wa makaa ya mawe wahakikishe wanatekeleza maelekezo yote waliyoelekezwa ili kulinda mazingira.” Bwa.Baruti

kwa upande wake Meneja wa Mazingira na Usalama wa Tancoal Bwa. Fericks Bida amesema kuwa, Kampuni inazingatia maelekezo wanayopewa na Baraza kwa kuhakikisha ulipuaji wa miamba unakuwa katika viwango vinavyokubalika isizidi mitetemo itakayoleta mazara kwa watu waliokaribu na mgodi. Kwa upande wa maji yanayotoka kwenye mgodi wanahifadhi katika mabwawa yaliyochimbwa kwenye mgodi ili kuepusha yasisambae na kweda kweye vyanzo vya maji.

Vile vile Bodi ya NEMC imetembelea Mto Luhuhu ambao unaotenganisha Mkoa wa Ruvuma na Njombe, katika ziara hiyo Bodi imebaini uchafuzi mkubwa wa mto huo na kupelekea mto kujaa udongo na kina cha mto kupungua pamoja na maji ya mto kubadilika rangi kuwa mekundu. Bodi ya Wakurugezi ya NEMC ipo kweye ziara katika Kanda ya Kusini kujionea hali ya kimazigira.

0/Post a Comment/Comments