Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb) (kulia) akieleza kuhusu umuhimu wa
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Zanzibar, kuongeza ushirikiano kwa Serikali
ya Zanzibar, ili kufanikisha utekelezaji wa Sera za Fedha, wakati alipotembelea
BoT tawi la Zanzibar, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kutembelea taasisi zilizo
chini ya Wizara hiyo visiwani Zanzibar, kushoto ni Naibu Gavana wa BoT, Dkt.
Bernard Kibesse.
Mkurungenzi Ofisi Ndogo ya BoT- Zanzibar, Dkt. Camillius Kombe, akielezea Sera ya Fedha inavyozingatia hali ya uchumi wa Visiwa vya Zanzibar, wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb) (hayupo pichani) na viongozi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Zanzibar,
Mkuu wa Kitengo cha
Uhasibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Zanzibar, Bi. Dyness Francis
Mdoe, akielezea jambo, wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb) (hayupo pichani) na viongozi wa BoT
katika tawi hilo, visiwani Zanzibar.
Na Benny Mwaipaja, Zanzibar
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Mhandisi Hamad
Yussuf Masauni, ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania kufanya tafiti mbalimbali
zitakazosaidia kukuza uchumi wa Zanzibar kupitia sekta za uchumi wa blue pamoja
na utalii.
Mheshimiwa Masauni ametoa maagizo hayo alipofanya ziara ya
kikazi kwenye Tawi la Benki Kuu ya Tanzania lililoko kisiwani Unguja-Zanzibar
ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kutembelea taasisi zilizochini ya Wizara
ya Fedha na Mipango.
Alisema kuwa Zanzibar inategemea uchumi wa blue ikiwemo masuala
ya uvuvi pamoja na sekta ya utalii kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake
hivyo utafiti katika Nyanja hizo utasaidia kubaini njia bora za kuharakisha
ukuaji wa uchumi wake kupitia Sekta hizo muhimu.
"Mazingira ya Uchumi wa Zanzibar ni tofauti na mazingira ya
uchumi wa Bara, kuna maeneo ambayo katika uchumi wa Zanzibar yamepewa
kipaumbele likiwemo suala la uchumi wa blue, na utalii, hivyo kuna
kila sababu Benki Kuu ya Tanzania kufanya tafiti katika maeneo hayo ili
kuishauri vema Serikali", alieleza Mhandisi Masauni.
Kwa upande wake Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aneyesimamia
uthabiti wa sekta ya fedha pamoja na kusimamia Tawi la Benki Kuu-Zanzibar Dkt.
Bernard Kibesse amemhakikishia Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa
MHandisi Hamad Yussuf Masauni kwamba maelekezo aliyoyatoa yatatekelezwa.
Alisema kuwa Benki hiyo tayari imeanza mchakato wa kufanya
tafiti mbalimbali zitakazo saidia kukukuza na kuimarisha uchumi wa Zanzibar
pamoja na kutekeleza sera za fedha kwa manufaa ya nchi hiyo na Taifa kwa
ujumla.
"Tumesikiliza maagizo yako hasa ya kufanya tafiti kuhusu
hali ya uchumi wa Zanzibar kwa kujikita zaidi katika uchumi wa Blue na utalii
maeneo ambayo ndiyo nguzo kuu za uchumi wa Zanzibar", alieleza Dkt.
Kibesse.
Naye Mkurugenzi wa BoT Tawi la Zanzibar Dkt. Camillius Kombe
alieleza kuwa Sera imara za fedga zimeiwezesha Serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar kuwa na uchumi imara pamoja utulivu wa mfumuko wa Bei ambao hivi sasa
hauzidi asilimia moja.
Alisema kuwa kumekuwepo na utulivu wa bei visiwani Zanzibar kwa
muda mrefu, ambao unatokana na Sera za Fedha kuwa na ufanisi kwa upande wa
Zanzibar na imetokana na BoT Zanzibar kutoa hali halisi na mikakati ya kukuza
uchumi na kuipeleka kwa watoa maamuzi.
Mwisho
Post a Comment