Dubai inapitia kipindi kigumu cha hali mbaya joto kali. Eneo hilo ndani ya Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) lina joto kali linalovuka mpaka nyuzi joto 50 na kuhatarisha maisha ya watu zaidi ya milioni 3 wanaoishi katika mji huo.
Hivi karibuni nchini Canada zaidi ya watu 500 waliripotiwa kufariki dunia kwa sababu ya joto kali.
Kuepuka madhara hayo UAE kupitia kitengo cha hali ya hewa kimekuja na teknolojia inayoweza kupunguza hali hiyo ya joto, na teknolojia hiyo ni utengenezaji wa mvua feki.
TEKNOLOJIA HIYO INAFANYAJE KAZI?
Ndege ndogo zilizotumika kwenye majaribio ya mpango wa mvua feki Dubai.
Kwa mujibu wa taarifa za kitengo cha hali ya hewa cha UAE ni kwamba, zimetengenezwa ndege ndogo maalumu zisizo na rubani (drones), ambazo zimewekewa nguvu maalumu ya umeme.
Ndege hizi zinatumwa angani kwenye mawingu zikifika huko zinaruhusu umeme ambao huleta mshituko ama kupiga shoti mawingu na kuyasukuma mawingu hayo kubadili muundo wake.
Kubadilika huko kunasababisha unyevu nyevu na maji maji ambayo yakidondoka ardhini yanakuwa mvua ambayo haina tofauti yoyote na mvua iliyozoeleka.
Mtaalam mbobezi anayefanya kazi kwenye mradi huo wa mvua feki Prof Maarten Ambaum, aliwahi kunukuliwa na BBC kuhusu mradi huo na miradi mingine ya mvua feki hasa wakati huu nchi hiyo ikikumbwa na joto akisema:
“Nchi hii ina mawingu mengi sana, kwa hiyo mpango uliopo ni kusukuma mawingu haya ya matone ya maji yaweze kushikamana kama nywele kavu wakati yatakapokutana na umeme.
"Matone haya yakiungana na kuwa makubwa, yanadondoka, yanapodondoka yanakuwa mvua," alisema.
#TIMESDIGITAL

Post a Comment