RAIS SAMIA ATOA MILL 100 KUBORESHA SOKO LA MACHINGA COMPLEX

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akizungumza na wafanyabiashara hao. 

................................... 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi Cha Shilingi Milioni 100 kwa ajili ya Ujenzi wa Paa la Kisasa la kuzuia Jua na Mvua kwa Wahanga 1,800 wa Soko la Kariakoo waliohamishiwa Machinga Complex.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amezungumza na wafanyabiashara hao  jijini Dar es salaam na kuthibitisha kupokea fedha hizo ambapo amesema baada ya Jana kuwatembelea na kuwasikiliza, Rais Samia ameona changamoto hiyo na hivyo ametoa Milioni 100 ili lijengwe Paa la Kudumu kwa Bati la Kisasa.

RC Makalla amewaelekeza Suma JKT ambao ndio wajenzi kuanza Ujenzi Mara moja ili Wafanyabiashara hao wafanye biashara bila kero.

Kuhusu suala la Meza, RC Makalla amesema tayari amepatikana Mkandarasi atakaejenga Meza za kisasa za kuhamishika kuendana na hadhi ya Soko.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameelekeza Viongozi wa Jiji la Ilala kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya Taka, Mifumo ya Maji, Mifumo ya umeme na wafunge Vizima Moto ili kukabiliana na majanga ya Moto.

0/Post a Comment/Comments