- Aagiza *waliojipa majukumu ya kunyemelea kukusanya Wrong Parking wasakwe Mara moja*.
- Ataka *TARURA na Wakurugenzi kutoa elimu na kuweka Vibao*.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amezielekeza *Halmashauri* kwa kushirikiana na *TARURA* kuhakikisha wanaweka *Vibao vya Wrong Parking* kwenye maeneo yasiyo rasmi kwa *maegesho* ili kuepuka uonevu.
*RC Makalla* amesema hayo wakati wa kikao alichohitisha baina yake, *Wakurugenzi wa Halmashauri na TARURA* kilicholenga kuondoa kero ya tozo ya *Wrong Parking.*
Aidha *RC Makalla* amesema kikao hicho wamekubaliana *tozo ya Wrong Parking itekelezwe kwa mujibu wa Sheria* lakini kwa mtu ambae ataonekana *alidhamiria moja kwa moja kuvunja Sheria* huku akisisitiza *Elimu iendelee kutolewa.*
Pamoja na hayo *RC Makalla* ameamua kuunda timu ya wataalam kwajili ya kuandaa *mfumo mzuri wa Mapato* ili kuhakikisha *kiasi Cha tozo kinacholipwa kinaenda moja kwa moja serikalini na muhusika anapatiwa risiti* ili kuepuka udanganyifu.

Post a Comment