Asema watekelezaji hawana weledi na kusababisha kero na taharuki.
Aitisha kikao Cha dharuracha Wakurugenzi na TARURA kujadili.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameonyesha kukasirishwa na *utaratibu usiofaa wa ukamataji wa magari* kwenye maegesho yasiyo rasmi *"wrong parking"* ambapo ameelekeza kuhitishwa kikao Cha pamoja baina yake, *Wakurugenzi wa Halmashauri na TARURA* ili kupatia ufumbuzi Jambo hilo.
*RC Makalla* amefikia hatua hiyo baada ya kupokea *Malalamiko* mengi ya Wananchi juu ya *utaratibu mbovu* unaotumika na kusema Kama kiongozi *hawezi kuruhusu Jambo hilo liendelee.*
Aidha *RC Makalla* amesema amebaini pia baadhi ya *vijana wanaofanya kazi hiyo wamekosa weledi na busara* na wengi wao wamekuwa *wakivizia* mtu afanye kosa ili wamuadhibu badala ya *kutoa elimu* ili makosa yasifanyike.
*Mheshimiwa Makalla* amesema hayo wakati wa uwekaji wa *Jiwe la Msingi kwenye Jengo la utawala la Manispaa ya Ubungo* ambapo ameipongeza Manispaa hiyo kwa *usimamizi mzuri wa fedha za Serikali na kuwataka Watumishi kutoa huduma Bora kwa wabanchi.*
Hata hivyo *RC Makalla* ameipongeza Manispaa hiyo kwa *ukusanyaji Mapato* Jambo linalopelekea waanze *kutekeleza miradi kwa Fedha za ndani* na pia kutumia *Force akaunti* kukamilisha miradi iliyokuwa ikisuasua ikiwemo Jengo hilo la utawala.

Post a Comment