SERIKALI YASHAURIWA KUFANYA MAPITIO YA SERA YA MIONGOZO UZALISHAJI.

Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mazingira Clara Makenya akizungumza katika kikao cha wadau wa chakula leo jijini Dar es salaam

Mbunge wa Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro Saasisha Mafuwe akizungumza katika kikao cha wadau wa chakula

Mkurugenzi Idara ya usalama na Chakula Wizara ya Kilimo Dkt Honest Kessy akizungumza katika kikao hicho cha wadau wa chakula jijini Dar es salaam

NA MUSSA KHALID DAR ES SALAAM 

Serikali imeshauriwa kufanya mapitio ya sera miongozo ya uzalishaji, na kuongeza jitihada za kuelimisha jamii hasa masuala ya Uwekezaji wa Kilimo ili  kusaidia kuepukana na janga la uhaba wa chakula Nchini itayosababisha njaaa kwa jamii. 

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam Dar es salaam na Mwenyekiti wa kikundi cha Wabunge Vinara wa usalama wa chakula –Food Safety Mbunge wa viti maalum  Neema Lugangira katika Ufungunguzi wa kikao cha wadau wa chakula ambapo amesema serikali haina budi kuboresha mifumo ya chakula kuanzia kwa wazalishaji,watunzaji kwenye maghala na walaji kwani chakula lazima kiangaliwe ili Afya ziwe bora. 

Lugangira amesema Nchi ya Tanzania bado baadhi ya maeneo yanakabiliwa na uhaba wa chakula hivyo kusababisha watoto kuwa na udumavu katika ukuaji wao na utapiamlo  kutokana na vyakula wanavyokula.

Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mazingira Clara Makenya amesema Kilimo cha sasa kimekuwa kikiathiri mazingira kutokana na wakulima kutumia madawa na viuatilifu hali inayopelekea siku hadi siku ardhi kupoteza mbolea yake ya asili na hivyo mazingira kuharibika na kusababisha uzalishaji ukipungua.

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya usalama na Chakula Wizara ya Kilimo Dkt Honest Kessy  amesema katika suala la uzalishaji bado limekuwa na changamoto kutokana na tija kuwa chini.

Saasisha Mafuwe ni Mbunge wa Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro amesema lengo lao ni kujadili na namna ya watanzania wanaweza kupata chakula chenye virutubisho vinavyohitajika ili kuweza kuondoa udumavu kwa watanzania.

Hata hivyo imeelezwa kuwa  kupitia kikao hicho na Mkutano Mkuu wa Chakula unaotararajiwa kufanyika Septemba mwaka huu New York Nchini Marekani wawakilishi watakaokwenda watakuja na suluhisho .

0/Post a Comment/Comments