Taarifa kutoka kwa uongozi wa Shule za Filbert Bayi inadaiwa kuwa uongozi wa shule hizo umetishia kulishitaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) baada ya kushindwa kulipa deni la zaidi ya shilingi milioni 76.
Inaelezwa kuwa deni hilo limetokana na mkataba wa kutoa huduma za viwanja, chakula, malazi na usafiri kwa timu za taifa za vijana na wanawake zilizoweka kambi katika shule hiyo iliyopo Kibaha kuanzia Machi 6, 2019 kwa gharama ya shilingi milioni mia tano ishirini na moja na laki nne na hamsini na tano.
Cc: itv

Post a Comment