Wananchi wa kata ya Nyakadua katika halmashauri ya wilaya ya Geita mkoa wa Geita ambao walikua wanapata shida kupata huduma za kijamii ikiwemo afya na shule kutokana na ubovu wa daraja linaunganisha kata mbili na uharibika mara kwa mara kutokana na mvua nyingi.
Hayo yameelezwa na Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa daraja kubwa linalojengwa na TARURA ambalo linathamani ya milioni 408 ambalo litakamilika ndani ya mwezi mmoja na litaanza kutumika.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA wilaya ya Geita Mhandisi Bahati Sabuye amesema daraja hilo limekamilika kwa jenga daraja lenye midomo mitatu yakupitishia maji hali itakayosaidia daraja hilo kukaa mda mrefu bila kusombwa na maji tofauti na makaravati husombwa na wingi wa maji yanayopita.
Kwa upande wake Naibu waziri wa TAMISEMI David Silinde ametoa mwezi mmoja mpaka kufikia tarehe 30 mwezi wa nane lianze kufanya kazi kusaidia wananchi.
Aidha ameongeza kua amefanya ukaguzi huo usiku ni kuangalia kama kazi bado zinafanyika au zimeisha simama na utakua ni utaratibu wa kukagua baadhi ya miradi hasa ya barabara maana ndio inayowatesa zaidi wananchi hasa madaraja ambayo hufanya wananchi kutembea umbari mrefu ili wavuke mito.

Post a Comment