Kituo cha kupozea umeme wa gridi kilichopo Unangwa mjini Songea
Jengo la TANESCO Mkoa wa Ruvuma
Baadhi ya watumishi wa TANESCO wakiongozwa na Meneja wa TANESCO
Mkoa wa Ruvuma Florence Mwakasege walipotembelea ofisi ndogo ya TANESCO Madaba
wilayani Songea
SHIRIKA
la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani
Ruvuma kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) limefanikiwa kusambaza umeme
katika vijiji 119 kati ya lengo la kusambaza umeme vijiji 161.
Meneja
wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Florence Mwakasege amesema mradi huo
umetekelezwa kupitia REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza ukihusisha pia ujenzi
wa njia mbili za umeme wenye urefu wa Kilometa 106 kuelekea kituo cha kufua
umeme wa maji Nakatuta Mto Ruvuma.
Amezitaja
gharama za mradi huo kuwa ni zaidi ya shilingi bilioni 43 na kwamba vijiji
ambavyo bado havijasambaziwa umeme utekelezaji wake upo katika hatua
mbalimbali.
Mhandisi
Mwakasege amesema tayari wateja 5,902 wa awali wameunganishiwa kati ya lengo la
kuunganishiwa wateja 6,178 mradi huo utakapokamilika kwa asilimia 100
Amesema
Mkoa wa Ruvuma una jumla ya vijiji 551,kati ya hivyo vijiji vyenye umeme ni 295,vijiji
visivyo na umeme vilivyoomba kupitia REA
awamu ya tatu mzunguko wa pili 256 na vijiji vitakavyokuwa na umeme baada ya
miradi inayoendelea kukamilika ni 295.
Hata
hivyo amesisitiza kuwa hadi kufikia Desemba 2022 vijiji vyote ambavyo
havijapatiwa umeme katika Mkoa wa Ruvuma vinatarajiwa kumfikiwa na umeme.
Kuhusu
upatikanaji wa umeme mkoani Ruvuma,Mhandisi Mwakasege amesema upatikanaji wa
umeme ni wa kuridhisha baada ya Mkoa kuunganishwa na Grid ya Taifa katika
Wilaya za Songea,Namtumbo,Mbinga,Nyasa na Tunduru.
“Mkoa
wa Ruvuma pia unapata umeme kutoka kwa wawekezaji binafsi wa Kampuni za Tulila na Andoya ambao wana uwezo wa kufua
umeme megawati 5.5 na kuingiza kwenye Grid ya Taifa’’,alisema Mwakasege.
Amewataja
wateja waliounganishiwa umeme katika kipindi cha Julai 2020 hadi Machi 2021
kuwa ni 7,411 ukilinganisha na lengo la mwaka la kuunganisha wateja 6,000 sawa
na asilimia 123.


Post a Comment