Mkurugenzi
wa Sensa na Takwimu za Jamii Ruth Minja akieleza jinsi Tanzania inavyoendelea
kudhibiti mfumuko wa bei ili kukuza uchumi na ustawi wa wananchi leo Julai 8,
2021 Jijini Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu mfumuko wa
bei wa mwezi June, 2021.Na Mwandishi wetu- Dodoma
Tanzania
imeendelea kufanya vizuri katika kudhibiti mfumuko wa bei wa Taifa ikilinganishwa
na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika
Mashariki kwa kipindi cha mwezi June , 2021.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ruth Minja leo Julai 8,
2021 Jijini Dodoma ambapo amesema mfumuko huo kwa hapa nchini
kwa mwezi Juni umefikia asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.3 mwezi Mei,
Kenya 6.32 kutoka 5.87 ya mwezi Mei, 2021 na Uganda 2.0 kutoka 1.9 mwezi
Mei, 2021 .
“Ongezeko
dogo la Mfumuko wa Bei hapa nchini kwa mwaka unaoishia Mwezi Juni, 2021
unamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei na huduma kwa mwaka unaoishia mwezi
Juni, 2021 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwaka
ulioishia mwezi Mei, 2021 na kwa nchi za
Afrika Mashariki Tanzania bado inafanya
vizuri”, alisisitiza Minja
Akifafanua
amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuchukua hatua za kudhibi
mfumuko wa bei ili kuwawezesha wananchi kuendelea kuchangia katika kukuza uchumi na shughuli nyingine za
maendeleo.
Baadhi
ya bidhaa zilizoongezeka bei kwa mwezi June ni; vitambaa vya nguo kwa asilimia
8.5, nguo za wanawake kwa asilimia6.3, viatu vya wanawake kwa asilimia 6.3,
viatu vya wanaume kwa asilimia 6.2, kodi ya
pango asilimia 4.9, vyakula kwenye migahawa asilimia 5.6 na gharama za
malazi kwenye nyumba za kulala wageni kwa asilimia 5.7
Kwa
upande wa bei za vyakula na vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi June,
2021 umepungua hadi asilimia 4.7 kutoka asilimia 4.9 kwa mwaka unaoishia mwezi
Mei , 2021.
Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa sheria ya
Takwimu Sura 351 na yenye mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji na
usambazaji wa Takwimu rasmi.
Post a Comment