Serikali imewatuma wahandisi wake kutoka TARURA kuzunguka nchi nzima kuangalia madaraja yote ambayo yameharibika na korofi ili yaweze kurekebishwa na kujengwa upya kusaidia wananchi kupata huduma mbalimbali za kijamii ambazo walikuwa wanashindwa kufika mahali kutokana na mawasiliano kukatika au kutokupitika vizuri hasa wakat wa Mvua.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde alipokua akikagua ujenzi wa daraja la iwelengula ambalo linajengwa kwa gharama ya zaidi ya milioni 428 chini ya mamlaka ya Barabara za mjini na Vijijini TARURA wilaya ya shinyanga katika kata ya Kitengula baada ya wananachi wa mtaa wa iwelengula kukosa mawasiliano kutokana na mvua kali zilizotokea mwanzoni mwa mwaka huu na kupelekea wananchi hao kushindwa kupata huduma mbalimbali za kijamii maeneo mengine kwa urahisi.
Kwa upande Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu ameishukuru TAMISEM kupitia TARURA kutoka kiasi cha shilingi milioni 428 kujenga daraja hilo kwa haraka kwani alilazimika kutoka bungeni katika vikao vya bajeti kuja kusaidia wananchi ambao walikua wanateseka kupata huduma hasa za afya kwani daraja hilo lilikua linaunganisha wanachi wa kata mbili tofauti amboa wanategemeana katika huduma mbalimbali.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA wilaya ya Shinyanga mhandisi Salvatory Yambi amesem ujenzi huo wanategemea utakamilika ndani ya miezi mitatu na kwasasa wamefikia hatua yakufunga nondo na ifikapo mwezi wa tisa basi daraja hilo jipya litapitika vizuri na limechelewa kuanza kujengwa kutoka na sababu za kiufundi ambao baadhi ya vifaa kuchelewa kufika kutoka kiwandani na maji kua mengi eneo hilo.




Post a Comment