WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WAASWA KUTENGA FEDHA KWA AJILI YA VITU VINAVYOWAGUSA WANANCHI

 












Naibu Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde ameagiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kutenga fedha katika mapato ya ndani wanayokusanya kuboresha sehemu za kazi za watumishi kwa kujenga nyumba za watumishi, madarasa na huduma zingine za halmashauri badala ya kutumia fedha hizo kwa vitu ambavyo haviwagusi wananchi moja kwa moja.


Kauli hiyo ameitoa baada ya kutembelea ujenzi wa nyumba sita za walimu ambazo zimejengwa na halmashauri ya manispaa ya Kahama mkoa wa Shinyanga katika shule ya msingi  Tungulu ambayo walimu walikuwa wakiishi katika nyumba mbovu za udongo na kuchangia ufaulu mdogo wa wanafunzi shuleni hapo.


Aidha Naibu waziri Silinde amesema ni aibu mpaka leo bado wanafunzi wanakaa chini au kwenye mawe darasani au kosomea chini ya miti kwa kukosa madarasa na kuagiza wakurugenzi ambao katika halmashauri zao kuna shida hizo watenge fedha kumaliza upungufu wa madawati na madarasa mapema iwezekanavyo.


Kwa upando wao Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga na Mkurugenzi wa manispaa ya kahama Anderson Msumba wameeleza sababu kubwa ya kufanikiwa kuwajengewa mazingira wezeshi watumishi wa manispaa ni kutengea fedha kila mwaka wa kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo nyumba na kuwawekea kila kitu ndani ili walimu wafundishe vizuri hata kama ni nje ya mji wajione kama wapo mjini na kwa mwaka huu wanakamilisha ujenzi wa nyumba zingine katika shule mbili za msingi.

0/Post a Comment/Comments