Picha kwa hisani ya Bbc
Jemima Okutu, kutoka nchini Kenya, amekuwa na tabasamu mwanana tangu Aprili 14, 2021, baada ya kupata watoto pacha.
Tabasamu lake siyo kwa kupata tu pacha, ila kwa kupata akiwa na umri mkubwa wa miaka 52 baada ya kuhangaika kwa miaka mingi.
Wakati wote sasa amekuwa na uso wa tabasamu anapowabeba watoto wake.
Ni nadra kwa wanawake wa umri wa aina yake kupata mtoto ama watoto, kwa sababu za kibaiolojia.
Jemima ni mzaliwa wa eneo la Magharibi mwa Kenya, ambapo akiwa msichana mdogo alitamani kwamba siku mmoja atajaliwa mume, kisha watoto. Ndoto hii yake haijatokea kama alivyopanga akilini mwake ila kwa sasa anashukuru tu kwa kujaaliwa watoto ambao muda huu wana miezi mitatu.
"Kitu ambacho ninaweza kukisema tu, ni 'ahsante kwa mwenyezi Mungu' . Nilikuwa nimefika mwisho wa kutafuta watoto, huu ni muujiza na kamwe sichukulii hali hii kuwa ya kawaida," anasema Jemima.
Cc: bbc


Post a Comment