Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam na Mwenyekiti wa Baraza hilo,Omari Kumbilamoto akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani
Kaimu
Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Tabu Shaibu akizungumza na waandishi wa
habari akitolea ufafanuzi kuhusu suala la TARURA
....................................................
NA MUSSA KHALID DAR ES SALAAM
Baraza
la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam limelazimika kusitisha
kikao cha baraza hilo baada ya Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na
Mijini (TARURA) kukosekana katika kikao hicho.
Hayo
yamejiri leo jijini Dar es salaam katika kikao cha kawaida cha baraza hilo kwa
lengo la kupitia taarifa za utendaji kazi wa jiji cha Robo ya nne ya mwaka.
Akizungumza
katika Kikao hicho Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam na Mwenyekiti wa
Baraza hilo,Omari Kumbilamoto amesema TARURA wametenga takriban Bill 10 kwa
ajili ya ujenzi wa barabara katika mkoa wa Dar es salaam lakini kuna baadhi ya
Kata barabara hazijajengwa.
‘Changamoto
kubwa na masikitiko ni kwamba TARURA kabla hawajatenga hizi fedha walitembelea
kata zote 36 wakakutana na madiwani na maafisa watendaji na serikali za mitaa
na wakawauliza madiwani kuwa ni kipaumbele kipi za barabara kwenye mitaa yao na
cha kustaajabisha na masikitiko kuna kata kama ya Chanika haijawekewa hata
barabara moja’amesema Meya Kumbilamoto
Aidha
Meya Kumbilamoto amesema kama inavyoelewaka kwa sasa madiwani hawahusiki na
matengenezo ya Barabara kwani zote zipo chini ya TARURA.
Katika
hatua nyingine Meya Kumbilamoto amesema wameadhimia walitenga kwenye bajeti yao
takriban Bill 2 kujenga madarasa 200 ya shule za sekondari hivyo amemuelekeza
Mkurugenzi kuwa hawatasubiri mpaka watoto wafaulu bali waanze mgawanyo wa fedha
mapema.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Tabu Shaibu amesema
katika Maazimio ya nyuma waliadhimia na walikubaliana TARURA waweze kubainisha
mapungufu na jambo lolote linalohusiana na barabara.
Hata hivyo Baraza hizo limeadhimia kuafanya kikao kingine baada ya shughuli za upokeaji wa mwenge Agost 18 mwaka huu.


Post a Comment