BARAZA VYAMA VYA SIASA LATAKIWA KUEPUKA MVUTANO NA TCD.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi wakati alipokutana na kuzungumza na safu mpya ya uongozi wa baraza la Vyama vya siasa nchni (picha na mtandao)
.............................................................. 

NA MUSSA KHALID DAR ES SALAAM 

Baraza la Vyama vya siasa nchini limetakiwa kuepukana na mvutano kati ya baraza hilo na baraza la kituo cha demokrasia TCD kwani wote kwa Pamoja wana jukumu la  kukuza demokrasia Nchini

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi wakati alipokutana na kuzungumza na safu mpya ya uongozi wa baraza hilo baada ya uongozi huo kupatikana katika uchaguzi uliofanyika julai 28 2021 Jijini Dodoma 

Jaji Mutungi amelikumbusha baraza hilo kuhakikisha linakuwa na mikakati ya kukuza demokrasi  na utawala bora ili kuendelea kukuza amani ya nchi.

Aidha Jaji Mutungi amesema baraza linawajibu  wa kuwaaminisha watanzania kwa vitendo juu ya dhana na uwepo wa demokrasia na utawala bora Nchini  na siyo kuwa na mvutano na baraza la kituo cha demokrasia TCD.

Juma Khatibu ni Mwenyekiti wa Chama Cha siasa Cha Ada Tadea Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya siasa,amesema Baraza hilo litaendelea kufanya siasa za kistarabu ikiwa ni pamoja na kuweka uzalendo mbele wa taifa ili kufanikisha maendeleo ya nchi na kuahidi  kuendeleza jitihada za kuwa kiungo bora kati yao na Seikali.

Baraza hilo jipya ya vyama vya siasa pia limezindua kamati ya uongozi ambayo itaanza kazi mara moja ya ujenzi wa Demokrasia na utawala bora nchini.




 

0/Post a Comment/Comments