CHANJO YA CORONA KUTOLEWA UWANJA WA UHURU JUMAPILI

 


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala amesema kuwa Mkoa huo utafanya zoezi la wazi la utoaji chanjo kwa wakazi wote siku ya Jumapili Agosti 22,Mwaka huu katika uwanja wa Taifa kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar es Salaam, amesema zoezi hilo litafanyika katika uwanja wa uhuru ambapo watu wote kuanzia miaka 18 watapata chanjo hiyo huku akidai hatua hiyo inatokana na kupokea malalamiko kutoka kwa watu ya kukosa chanjo hiyo.

Aidha amesema  hatua hiyo ni kuhakikisha kuwa wanaofanya kazi kupata nafasi siku za mapumziko.


Katika hatua nyingine amewaagiza Wakuu wa wilaya zote za Dar es salaam kuweka siku moja ambayo itawaruhusu Watumishi wote na Wananchi kupata chanjo kwa hiari yao kuwezesha Watu wengi kupata chanjo.

 

Hata hivyo amewataka  wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya wimbi la tatu la mlipuko wa virusi vya corona(Delta).

0/Post a Comment/Comments