Kuna mfumo wazi juu ya uongozi ndani ya Kundi la Taliban.
Mawlawi Hibatullah Akhundzada amekuwa kiongozi mkuu wa kundi hilo tangu mwaka 2016. Msomi huyo wa kidini ndiye mwenye mamlaka kuu katika masuala yote ya kisiasa, dini na kijeshi.
Anaungwa mkono na manaibu watatu na mawaziri kadhaa ambao husimamia vitengo vya kijeshi, ujasusi na uchumi.
"Rahbari Shura," anayejulikana pia kama "Quetta Shura," ndiye mwenye mamlaka ya juu zaidi ya ushauri wa kundi hilo lenye washirika 26.
Tawi la kisiasa la Taliban ambalo linaliwakilisha kundi hilo kimataifa liko mjini Doha, Qatar. Masuala ya siasa yanaongozwa na mwanzilishi mwenza wa Taliban Mullah Abdul Ghani Baradar. Hii ikiwa ni sehemu ndogo tu ya kundi la Taliban ambayo imeshughulikia mazungumzo ya amani na Marekani.
#TimesFMDigital


Post a Comment