JAMII ZAASWA KUWEKEZA KWENYE MISITU

 













Na Mwandishi Wetu

Katika kukabiliana na Mabadiliko ya tabia ya nchi Jamii imeshauriwa kuchangamkia fursa za Uwekezaji katika sekta ya Misitu nchini ili kuhakikisha wanalinda uoto wa Asili wa  misitu pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya nchi.

Wito huo Umetolewa Jijini Dar es salaam na Bwana Kikolo Mwakasungura Kaimu Mkurugenzi wa African Forest Wakati wa Mkutano  na Wadau tofauti wa  wawekezaji wa sekta ya Misitu wanao ishi mijini .

Mwakasungura amesema kuwa Mkutano huo Umelenga kuwakutanisha wadau wa Misitu hasa wanao ishi Mijini  ili waweze kuchangamkiwa fursa ya   kuwekeza katika sekta hiyo  Muhimu nchini hasa  maeneo ya Vijijini.


Aidha amesema kuwa kila mtu anauweo wa kuwekeza kwenye misitu hata kwa kuanza na hekalu moja.


"Suala la kuwekeza kwenye misitu ni la kila mtanzania na kwa hapa Nchini mikoa ya nyanda za juu kusaini ndiyo sehemu zinazostawi Zaidi ikiwemo Mbeya,Iringa,Songea,Njombe na Makete ni maeneo yanayostawi zaidi"alisema Mwakasungura


Kwa upande wao baadhi ya Wawekezaji katika sekta ya Misitu waliohudhuria mkutano huo wameiomba Serikali  kuhakikisha wanakabiliana na changamoto ya Uchomaji moto wa Misitu ambayo kwa sasa imekisili  katika Maeneo ya Vijijini

0/Post a Comment/Comments