JATU YAWAASA WAKULIMA KUACHA KILIMO CHA MAZOEA

 

Mkurugenzi Mtendaji wa JATU PLC Bw.. Peter Isare akizungumza  na wadau wa Kilimo katika mkutano Mkuu wa Wakulima wa JATU PLC uliofanyika katika ukumbi wa Mkutano Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam ambapo alitoa matokeo ya hisa walizoingiza sokoni. Wadau wa Kilimo wakifuatilia wakiwa katika mkutano Mkuu wa Wakulima wa JATU PLC uliofanyika katika ukumbi wa Mkyano Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Mbatilo)

*********************************

Wakulima nchini wametakiwa kuachana na kilimo cha mazoea  na kufanya kilimo biashara hasa katika kuongeza tija ya uzalishaji ili kukabiliana na changamoto wakati bei inaposhuka pamoja na kuweka kumbukumbu na kuwasiliana na wanunuzi kabla ya kulima mazao yao. 


Kilimo cha biashara kinafanywa na watu binafsi, kampuni mbalimbali na taasisi zilizojipambanua kwa ajili hiyo ikiwemo kampuni ya Jatu iliyofanya uwekezaji ya kilimo cha mazao mbalimbali kwa ajili ya biashara.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa mwaka Mkurugenzi mtendaji wa JATU.l, Peter Gasaya amesema jatu imewekeza katika mikoa mbalimbali nchini na tayari  taasisi hiyo imeorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na malengo yake kwa kipindi cha mwaka huu ni kukusanya kiasi cha zaidi ya Shilingi bilioni 7.5 zitakazoisaidia kuongeza tija katika kilimo ikiwemo ununuzi wa zana mbalimbali ,

Kampuni hiyo imewekeza kwenye mashamba yenye ukubwa wa zaidi ya hekari 17,678 katika mikoa ya Manyara, Morogoro, Tanga, Ruvuma, Singida na Njombe.

Aidha kupitia mashamba kampuni ya JATU  wamekuwa wakizalisha takribani tani 8,670 za nafaka ambazo huchakatwa katika viwanda vidogo vidogo walivyoanzisha mkoani Morogoro na Dodoma

0/Post a Comment/Comments