1.
Kamati ya Kudumu ya Baraza la
Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Zanzibar, wakipata
maelezo kutoka kwa Bi.Maimuna Salum Mkurugenzi wa Mazingira na Taka Hatarishi
Tindwa Medical and Health Service Kisarawe Mkoa wa Pwani
1.
Kamati ya Kudumu ya Baraza la
Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Zanzibar,
wakiangalia shimo la mabaki ya majivu yaliotokana na taka hatarishi
zilizochomwa kiwandani hapo.
1.Waziri Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
Zanzibar Mhe. Saada Mkuya (katikati), akizungumza baada ya kufanya ukaguzi
pamoja na kamati ya kudumu ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za
Viongozi katika kiwanda cha Tindwa
Medical and Health Service kilichopo Kisarawe Pwani.
1 Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Zanzibar,
wakisikiliza maelezo yanayotolewa na Waziri Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
Mhe. Saada Mkuya (hayupo pichani).
Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Kudumu ya
Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Zanzibar
yafanya ziara Kisarawe Mkoa wa Pwani kwenye mitambo ya kuchomea taka hatarishi
katika Kiwanda cha Tindwa Medical and Health service, ili kujionea namna
wanavyochoma taka hizo bila ya kuathiri Mazingira.
Kamati hiyo imeambatana
na Waziri Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mhe. Saada Mkuya, Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Dkt. Omary Shajaak, Makamu
Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Mtumwa Peya pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Mhe.Saada Mkuya amesema
kuwa lengo la kufanya ziara ni kujifunza jinsi gani wanaweza kutunza na
kuteketeza taka hatarishi kutoka Hospitalini na Viwandani bila ya kuathiri
mazingira. Ameeleza kuwa kwa upande wa Zanzibar kuna changamoto kubwa katika
kuteketeza taka hatarishi hivyo wametumia fursa hii kuja kujifunza namna gani
watachoma na kuteketeza taka hizo.
"kwa upande wa
Zanzibar tuna changamoto kubwa katika kuhifadhi na kuteketeza taka hatarishi kwa
mfano tuna Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja ambayo ndio pekee inateketeza taka hizo
na muda mwengine kupelekea kuelemewa na kushindwa kufanya kazi zake kwa
ufasihi”. Amesema Mhe. Saada
Ameendelea kusema kuwa
Zanzibar ni kisiwa cha utalii na inafahamika kuwa utalii unaendana na hali ya
mazingira na usafi na kama tutashindwa kuhifadhi na kutunza mazingira yetu kwa
kiasi kikubwa tutapunguza ubora wa utalii. Hivyo tumekuja hapa kujifunza na
itatusaidia kuweka miongozo ya namna gani ya kuhifadhi na kuteketeza taka hizo
bila ya kuharibu mazingira.
Kwa upande wake Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za
Viongozi Wakuu wa Kitaifa Zanzibar Mhe. Mtumwa Peya amesema kuwa, ziara hii ya
kamati katika kiwanda cha Tindwa imewapa fursa ya kujifunza kwani kwa upande wa
Zanzibar bado kiwanda kikubwa cha kuunguza taka hatarishi bado hakipo.
“Kwa upande wetu
Zanzibar hatuna kiwanda kama hiki hivyo kupelekea taka kuzagaa hovyo na
kuharibu mazingira, mimi nikiwa kama kaimu Mwenyekiti wa Kamati hii
nimefarijika sana kuona kiwanda hiki namna wanavyoteketeza taka hatarishi. Sisi
ni viongozi wa kusimamia Serikali hivyo tutaenda kuishauri Serikali yetu ili
tuweze kuwa na namna bora ya kuchoma taka hatarishi kama tulivyojifunza hapa”. amesema
Mhe. Mtumwa
Naye Bi.Maimuna Salum
Mkurugenzi wa Mazingira na taka hatarishi
Tindwa Medical and Health service, amesema kuwa kiwanda kinafanya kazi kwa
kushirikiana na Taasisi za Kiserikali ikiwemo Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali,
TMDA, OSHA pamoja na NEMC ili kuweza kufanya kazi zao kwa uweredi na kuzingatia
matakwa ya Sheria ya Nchi.
Ameeleza kuwa Tindwa inajishughulisha
na uteketezaji wa taka hatarishi kutoka Hospitali na Viwandani na wamefanikiwa
kwa kiasi kikubwa kuteketeza taka japo changamoto waliyonayo kwa sasa ni baadhi
ya kemikali kushindwa kuteketezwa kutokana na uwezo mdogo wa mashine
walizonazo. Aidha ameeleza kuwa kila penye changamoto fursa ipo hivyo kama
kiwanda wamejipanga kuongeza uwezo wa mashine ambazo zitaweza kuteketeza taka
hizo ambazo mashine ya sasa imeshindwa.




Post a Comment