Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Gerald Kusaya akizungumza katika Hafla ya utiaji saini wa hati ya Makubaliano kati ya serikali na Sekta katika kudhibiti uchepushaji wa kemikali bashirifu na Dawa Tiba (picha na maktaba)
.......................................................
NA MUSSA KHALID DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za
Kulevya (DCEA) kwa
kushirikiana na Mamlaka nyingine za serikali pamoja na sekta binafsi
imetekeleza mradi wa Pamoja chini utaribu wa Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti
Dawa za Kulevya ili kuimarisha na kuzuia Uchepushaji wa Kemikali Bashirifu na
Dawa Tiba zenye Asili ya kulevya.
Akizungumza katika Hafla ya utiaji saini wa
hati ya Makubaliano kati ya serikali na Sekta katika kudhibiti uchepushaji wa
kemikali bashirifu na Dawa Tiba,Kamishna Generali wa Mamlaka hiyo Gerald Kusaya
amesema lengo la mradi huo ni kuweka utaratibu wa kufanya kazi kwa pamoja.
Kusaya amesema ushirikiano huo utachangia
kuboresha zaidi utekelezaji wa matakwa ya sheria zilizopo kwa wadau wa serikali
kuwa na jukwa na kufanya kazi na kuongeza uzoefu katika taarifa mbalimbali za
udhibiti.
‘Kwa siku ya leo Mkataba huu wa makubaliano
ya ushirika katika kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu utaanza na
kampuni chache takriban 32 na vyama viwili 2 vya wadau wanaojishughulisha na
dawa tiba zenye asili ya kulevya ambavyo ni TPMA na TAPI wakiwakilisha kampuni
zinazofanya kazi hizo’amesema Kusaya
Afisa mauzo kutoka Taasisi binafsi ya
Kemikali Charles Fubusa amesema watahakikisha wanashirikiana pamoja na Mamlaka
za kiserikali ili kuendelea kupata mwongozo utakao waletea manufaa.
Churchill Katwaza ni Mwenyekiti wa taasisi TAPI
inayojishughulisha na uagizaji na usambazaji wa dawa,vitendanishi pamoja na
vifaa tiba,ameahidi kuwa watashirikiana
kuhakikisha udhibiti wa dawa na kemikali haziendi nje ya utaratibu uliopanga.
Katika hafla hiyo ameshiriki Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt Fidelis Mafumiko ambapo amezikumbusha Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba kuwa zina majukumu ya kusimamia kemikali bashirifu zote za viwandani na majumbani na dawa tiba zenye asili ya kulevya katika matumizi yake.

Post a Comment