Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na
aliyekuwa Waziri katika serikali ya Awamu ya Nne, Profesa Mark Mwandosya
(kulia) na mkewe Lucy Mwandosya (wa pili kulia) wakati alipowasili
kwenye viwanja vya Chuo cha Ufundi cha wilaya ya Busokelo mkoani Mbeya kuzindua
Chuo hicho, Agosti 1, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Chuo cha
Ufundi Stadi cha wilaya ya Busokelo mkoani Mbeya, Agosti 1, 2021.
Wengine pichani kutoka kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, Waziri wa Elimu,
Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni Mbunge wa
Busokelo, Atupele Mwakibete. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazma kaunda
suti wakati alipotembelea darasa la mafunzo ya ushonaji nguo katika Chuo cha
Ufundi Stadi cha wilaya ya Busokelo mkoani Mbeya, Agosti 1, 2021.
Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Agosti 1, 2021
amekabidhiwa zawadi ya picha aliyopiga akivuka mto Rufiji kwa kutumia ngalawa
mwaka 2010 akiwa Mkuu wa wilaya ya Rufiji wakati alipompokea Profesa
Mark Mwandosya aliyekuwa ni Waziri katika serikali ya Awamu ya
Nne. Picha hiyo ilikabidhiwa kwake na Profesa Mwandosya (kushoto) na
mkewe Lucy Mwandosya (wa pili kushoto) baada ya Mheshimiwa Majaliwa kuzindua
Chuo cha Ufundi Stadi cha wilaya ya Busokelo mkoani Mbeya. Wa
pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Post a Comment