RC MAKALA KUIZUNGUKA DAR NZIMA KUTATUA MIGOGORO

 




Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* anatarajiwa kuanza rasmi *ziara ya kusikiliza na kutatua kero na changamoto za Wananchi* wa Mkoa huo Jimbo kwa Jimbo ikiwa ni Mpango wake wa kupatia *ufumbuzi kero za Wananchi.*


*RC Makalla* amesema ziara hiyo itaanza rasmi *Jumatatu ya August 30* kwenye *Jimbo la Kawe Viwanja vya Tanganyika Packers*, August 31 *Jimbo la Kibamba*, September 01 *Jimbo la Segerea,* September 02 *Jimbo la Mbagala* na September 03 *Jimbo la Kigamboni* ambapo zoezi litaanza kuanzia *Saa mbili Asubuhi Hadi majira ya jioni.*


Aidha *RC Makalla* amesema kutakuwa na *jopo la Wataalamu wabobezi* wakiwemo *Watendaji wa Serikali, Wanasheria, Kamishina wa Ardhi, Maafisa Ardhi, Jeshi la Polisi, TAKUKURU na Wadau wote* wanaojihusisha na masuala ya kisheria.


Pamoja na hayo *RC Makalla* ametoa *wito kwa Wananchi* wote Wenye Migogoro kutumia Fursa hiyo *kuwasilisha Malalamiko yao ili yaweze kupatiwa ufumbuzi kwa mujibu wa Sheria.*

0/Post a Comment/Comments