Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na (SMZ), Bw. Emmanuel
Mpawe Tutuba (katikati) akiongoza Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara
ngazi ya Makatibu Wakuu chenye wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano
(SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Kulia ni Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango na Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Bi. Mary Ngelela Maganga. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 02/08/2021
katika Ukumbi wa Reform – uliopo
katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Wajumbe wa Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na
Biashara ngazi ya Makatibu Wakuu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kukamilika kwa kikao kazi cha Maandalizi ya Kikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT
na SMZ ya Kushughulikia Masuala ya Muungano. Katikati ni Mwenyekiti wa Kikao
hicho Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango (SMT), Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba.
Wengine katika picha, wa pili kutoka kulia ni Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango (SMZ) na Bw. Amour Hamil Bakari, Katibu Mkuu, Wizara
ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (SMZ), Bi. Mary Ngelela Maganga, Katibu Mkuu,
Ofisi ya Makamu wa Rais (SMT) na Bw. Khalid Hamrani Mkurugenzi, Idara ya
Uratibu wa Shughuli za Serikali – Zanzibar.
Post a Comment