Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Yuda Thadeus Ruwaichi, amewaagiza mapadri wote wanaohudumu Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwenda kupata chanjo ya Covid-19.
Amewataka waamini Wakatoliki wenye kustahili kuchanja, wafanye hivyo kulinda afya zao.
Amewataka kuwapuuza wanaoshabikia watu wasichanjwe kwa kelele zao.
"Kipindi tete. Nawahimza yafuatayo, zingatieni maagizo ya wataalamu wa afya. Tieni bidii ya kuyafanyia kazi.
“Nawaalika wenye umri wa kustahili kuchanjwa mkachanjwe. Najua kuna maneno mengi, lakini Baba Mtakatifu Francis katangulia kuchanja, nami nimewapa mfano nimekuwa wa kwanza kuchanja.
“Mwaka jana tuliomba Mungu atujalie tupate chanjo na imepatikana. Ajabu tumeanza malumbano. Tutumie fursa tunitunze na kujihami.
“Natoa agizo kila padri akachanjwe. Tuache utoto na mzaha. Wale wanaopiga kelele za akina Gwajima, achaneni nao! Yawekeni pembeni. Tujihami. Na tuendelee kumwomba Mungu atunusuru na hili janga!”
#TimesFMDigital

Post a Comment