Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa UTT
AMIS, Bw. Simon Migangala, akielezea vyanzo vya mapato ya taasisi hiyo, wakati
wa ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf
Masauni (Mb) (hayupo pichani), katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (katikati) akisikiliza maelezo kuhusu
mitambo ya kuhifadhia taarifa za wateja wa Mfuko wa UTT AMIS, alipotembelea
taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango
Mheshimiwa Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, ameiagiza Kampuni ya Uwekezaji ya
Pamoja-UTT-AMIS kutoa elimu zaidi ya uwekezaji kwa wananchi wakiwemo wastaafu
wanaokabiliwa na changamoto kubwa ya kufanya uwekezaji wa mafao yao ya uzeeni
kwenye miradi isiyo na tija na kuwasababishia hasara.
Mheshimiwa Masauni alitoa maagizo
hayo alipotembelea Taasisi ya UTT-AMIS inayosimamiwa na Wizara ya Fedha na
Mipango, ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake katika Taasisi zinazosimamiwa na
Wizara hiyo, Jijini Dar es Salaam
Alisema kuwa uwekezaji kwenye mifuko
inayosimamiwa na UTT-AMIS umekuwa na tija kubwa na kwamba licha ya mfuko huo
kufanya vizuri na kutoa faida inayomnufaisha mwekezaji, watu wengi hawana
taarifa muhimu kuhusu mfuko huo na kuuagiza uongozi kuongeza kasi ya
kujitangaza.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa
Mfuko huo unaoendesha mifuko 6 ya uwekezaji, ukiwemo mfuko wa Umoja, Wekeza,
Watoto, Jikimu, Ukwasi na Hati Fungani, Mkurugenzi Mtendaji wa UTT-AMIS, Bw.
Simon Migangala, alisema kuwa mfuko wake umefanikiwa kuongeza mtaji kutoka
shilingi bilioni 290.7 hadi shilingi bilioni 619.6 katika kipindi cha miaka
miwili iliyopita.
Mwisho
Post a Comment