MISS EAST AFRICA 2021, YATOA MILIONI 146




Makamu wa Rais wa mashindano ya urembo ya mrembo wa Afrika mashariki (miss east Africa)  beaut pageant Joyl Mtesi akizungumza na waandishi wa habari


Wa kwanza kulia ni Rais wa mashindano ya urembo ya mrembo wa Afrika mashariki (Miss East Africa) Beaut pageant Callist akizungumza na waandishi wa habari.



Gari aiana ya Nissan X trail litakalotolewa  zawadi kwa mshindi.



Na Richard Mrusha

Jumla ya zawadi zenye thamani ya shilingi Milioni Mia moja arobaini na sita 146,000,000 zitatolewa katika mashindano ya mwaka huu ya Miss East Africa 2021


Hayo yamesemwa na Rais wa mashindano ya urembo ya mrembo wa Afrika Mashariki( Miss  East Africa Beauty Pageant RENA CALLIST


CALLIST amesema Mshindi kwanza wa mashindano hayo atazawadiwa gari jipya la kisasa aina ya Nissan x Trail,toleo la Mwaka 2021/21 lenye thamani ya shilingi 110,000,000.


Amesema mshindi wa pili atapata pesa taslim shilingi 11,000,000 na mshindi wa tatu atajipatia lesa taslim shilingi 5,000,000.


Amesema kutakuwa na zawadi zingine mbalimbali kwa washiriki wa mashindano hayo zenye thamani ya shilingi milioni ishirini na jumla ya nchi 16 za ukanda wa Afrika Mashariki zimethibitisha kushiriki mashindano hayo ambayo yatafanyika Tarehe 26- 11-2021 jijini Dar es salaam na yameandaliwa na Rena Events Limited ya Jijini Dar es salaam.


Nchi zilizothibisha kushiriki Mashindani hayo ni Tanzania,Kenya,uganda,Rwanda,Burundi, South Sudan,Ethiopia,Elitrea,Djibouti,Somalia,Malawi,Visiwa vya Seychelles,Comoros,Madagascar,Reunion na Mauritius "Calist amesema"


Amesema Mashindano ya Mwaka huu yanatarajiwa kurushwa moja kwa Moja na kuangaliwa na watazamaji zaidi ya  mia tatu kupitia Telelevision na internet Dunia nzima ambapo Tanzania itafaidika na mashindano hayo moja kwa moja kwa kutangaza vivutio vya utalii fursa za uwekezaji wa Biashara pamoja na utamaduni kwa ujumla.

0/Post a Comment/Comments