Jeshi
la Polisi kanda
Maluum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata
watu 13 wa makosa ya kujipatia
pesa kwa njia za udanganyifu (utapeli) wa madini bandia.
Akitoa
taarifa hizo kwa
waandishi wa habari
leo jijini Dar es
Salaam Kamanda wa Polisi
wa Kanda Maalum ya Polisi ACP
Muliro Jumanne Muliro amesema
watuhumiwa hao wamekamatwa
katika operasheni kali inayoongozwa
na taarifa fiche inayolenga kuzuia
vitendo vya kihalifu na kuwakamata wale
wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Kamanda
Muliro amesema watuhumiwa hao
wamekamatwa Augusti 20 2021 katika maeneo ya Mbezi
Makonde Wilayani Kinondoni huku akiwataja
watuhumiwa hao wakiongozwa
na Christopher Robert@Mayanga,(29),Mkazi wa Tabata Bima, Harold
Martin@Pouwes,(60) raia Afrika Kusini na wenzao kumi na moja kwa tuhuma za uuzaji wa madini bandia.
Aidha Jeshi
la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limeyakamata na
kuyachunguza magari hayo 6, ambayo yalikuwa yakitumiwa
na watuhumiwa hao
amabayo ni gari
namba T 479 Dhw Toyota Prado, T 740
Dsw Toyota Alphard,
T 273 Dhm Toyota Noah, T 241 Dvu
Mercdes Benz, T 751 Dk Toyota Racts Na T
974 Dmr Toyota Brevis.
Katika
tukio la pili, Jeshi la polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watu
wanne kwa tuhuma za kutenda makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu na kuiba /
kupora pikipiki toka kwa waendesha
pikipiki maarufu bodaboda.
Amewataja
watuhumiwa hao kuwa
ni Hizza Herbert (52), Mkazi
Tabata, Richard George (45), Mkazi wa Buguruni , Arif Henry (21), Mkazi wa
Buguruni, Saad Mohamed (25), Mkazi wa Mburahati.
Tayari
Baadhi ya pikipiki hizo zimeshatambuliwa na wamiliki halali huku Watuhumiwa
wote watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Post a Comment