PROGRAM YA MUSEAM ARTS EXPLOSION YAENDELEA KUWA KIVUTIO KWA VIJANA WA KITANZANIA.


Mkuu wa Idara ya Program inayoendesha Program ya Museam Arts Explosion kutoka Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni bw.Chance Adam Ezekiel akizungumza kuhusiana na Program ya Museam Arts Explosion ambayo hufanyika kila ijumaa ya mwisho wa mwezi.

NA MUSSA KHALID DAR ES SALAAM

Watanzania wametakiwa kupenda kutembelea kwenye vivutio vya utalii vilivyobeba urithi wa nchi ili kufahamu historia yake ilipotoka na inapokwenda na ilipo.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Idara ya Program inayoendesha Program ya Museam Arts Explosion kutoka Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Chance Adam Ezekiel wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii akieleza kuhusiana na Program ya Museam Arts Explosion ambayo hufanyika kila ijumaa ya mwisho wa mwezi.

Chance amesema pindi mtu akitaka kujua urithi wa nchi ni vyema akatembelea maeneo mbalimbali ya makumbusho pamoja na malikale zilizopo nchini kwani ndimo historia za nchi zimeandikwa.

‘Imekuwa ni changamoto kwa wanafunzi wengi wanaosoma masomo ya historia hawatembei kujifunza kwa nadharia na vitendo bali wanakariri jambo ambalo wanashindwa kuwa na uelewa mkubwa’amesema Chanche

Awali  Mkuu huyo wa Idara ya Program ya Museam Arts Explosion akieleza kuhusiana program hiyo,amesema malengo yao ni kuhakikisha wanainua na kukuza vipaji vya vijana wa kitanzania waweze kuufahamu urithi wa utamaduni kupitia sanaa zao.

‘Sisi tuna shughulika zaidi na wale wasanii wadodo na wanaochipukia kwa kuwakutanisha katika jukwaa moja na wanafanya maonyesho ambapo tangu mwaka 2016 tumefanya na wasanii wengi sana na hicyo wamejipatia mafanikio kwani tunaaalika watu wengi wakiwemo mabalozi na kutoka serikalini’ameendelea kusisitiza

Michael James ni Muandaaji wa Mchezo wa jukwaani wa Zama amesema lengo la kufanya mchezo huo ni kuwaelimisha watanzania ili waweze kuachana na tamaduni za kale zilizopitwa na wakati zinaikandamiza jamii ya kitanzania.

Hata hivyo vijana wametakiwa kuepuka kuiga maadili ya nje ya nchi badala yake wafate na kupenda kuishi kulingana na maadili ya kitanzania ili kuendelea kukuza utamaduni wao.

0/Post a Comment/Comments