PWANI WAPOKEA MWENGE WA UHURU

 


Mkoa wa Pwani unatarajiwa kupokea mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 Agusti 11, ukitokea Mkoani Morogoro.

Mapokezi hayo yataongozwa na mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, na  miradi mbalimbali ya maendeleo itazinduliwa katika Halmashauri zote saba za Mkoa huo.


Mwenge wa Uhuru mwaka huu unabeba kaulimbiu isemayo "Tehama ni Msingi wa Taifa endelevu, itumike kwa usahihi na uwajibikaji". 


Aidha mbio hizo zinahamasisha mapambano dhidi ya rushwa, mshikamano wa kitaifa na uwajibikaji wa pamoja, ujenzi wa jamii yenye Afya imara kwa kuzingatia lishe Bora, kuchukua hatua katika mapambano dhidi ya malaria na kuitokomeza na elimu sahihi juu ya dawa za kulevya na kubotesha huduma kwa waraibu wa dawa hizi.


Mbio hizo zinaanzia katika Wilaya ya Bagamoyo kisha kufuatia Wilaya za Kibaha , Kisarawe, Kibiti, Utete(Rufiji) na kuhitimisha mbio hizo katika Wilaya ya Mafia kabla ya kupokelewa  katika Wilaya ya Temeke.

0/Post a Comment/Comments