Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert
Ibuge akikagua moja ya mabanda ya maonesha kwenye tamasha la Majimaji Selebuka
mjini Songea
Mkuu wa Mkoa wa Lindi mheshimiwa Zainabu Telaki akiwa na
mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge
wakibadilishana mawazo na Chifu wa Tano wa Kabila ya Wangoni Chifu Imanuel Zulu
mara baada ya kufungwa Tamasha la Majimaji Selebuka katika uwanja wa Majimaji
mjini Songea
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge
akicheza ngoma ya Lizombe katika uwanja wa Majimaji mjini Songea siku ya
kufunga Tamasha la Majimaji Selebuka ambalo limefanyika kwa siku nane
...............................................
MKUU
wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ametoa rai kwa wadau wa
watalii kuvitangaza vivutio vilivyopo ukanda wa kusini ili kufungua milango ya
uwekezaji.
Ametoa
rai hiyo wakati anafunga tamasha la
Majimaji Selebuka ambalo limefanyika kwa siku nane kwenye uwanja wa
michezo wa Majimaji mjini Songea.
“Tumezoea
sana kutangaza vivutio kutoka kaskazini na
fukwe zilizopo Mashariki mwa nchi yetu, uwekezaji kusini unahitaji
juhudi za pamoja wadau na wananchi wa Kusini ili Southern Circuit yaanik Mzunguko wa Kusini
kwa hakika utangazwe vema’’,alisisitiza
RC Ibuge.
Amesema
kinachotafutwa hivi sasa ni kuongeza mapato kupitia sekta ya utalii na
kuhakikisha kuna uendelevu wa kutambulisha vivutio vya kusini Duniani.
Brigedia
Jenerali Ibuge amesema kuna soko kubwa la sekta ya utalii hivyo juhudi kubwa katika kutangaza vivutio vya
utalii zinaweza kuongeza uthaminishaji wa maliasili zilizopo na kuongeza kipato
kwa wabunifu na wananchi.
Hata
hivyo Mkuu wa Mkoa ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kulitendea
haki tamasha la Majimaji Selebuka mwaka huu ambapo ameagiza kuongeza juhudi
zaidi katika kuhakikisha matamasha yajayo
yanakuwa na ushiriki mkubwa na kuongeza vikundi vya ushiriki kutoka
mikoa ya Ruvuma,Lindi na Mtwara.
Katika
Hatua nyingine RC Ibuge amewakumbusha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya
kujikinga na UVIKO 19 kwa kuzingatia maelekezo yote yanayotolewa na wataalam wa
afya.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Zainabu Telaki akizungumza kwenye
tamasha hilo ametoa rai kwa wadau wa
utalii kuhakikisha kuwa vivutio vyote vilivyopo kwenye mikoa mitatu ya kusini
vinatangazwa kwenye luninga zote zilizopo nchini ili kufungua fursa za utalii
kusini.
Awali
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema akizungumza kwenye tamasha hilo
amesisitiza vivutio adimu vya utalii vilivyopo kusini ambavyo havipatikani sehemu nyingine
duniani vitangazwe kitaifa na kimataifa
kuvutia wawekezaji.
Mgema
ametoa rai kwa Bodi ya Utalii Tanzania kuhakikisha kuwa vivutio vya kusini
vinakuwa sehemu ya vivutio vinavyotangazwa ili watalii wengi waweze kufika
mikoa ya kusini kuangalia vivutio hivyo.
Amesema serikali tayari imeimarisha miumbombonu katika mikoa ya kusini hivyo watalii wanaweza kufika kusini kwa kutumia usafiri wa anga,barabara na majini.
Post a Comment