- *
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amefanikiwa kupatia ufumbuzi hali ya sintofahamu iliyokuwa ikikabili *Mradi wa Ujenzi wa Soko la Kisasa la Tandale* lenye thamani ya *Bilioni 8.7* baada ya Ujenzi huo kusimama kwa muda Kutokana kutoka kile kilichodaiwa kuwa *Mkandarasi amecheleweshewa malipo.*
Mapema leo *RC Makalla* amekagua Mradi huo na kufanya *kikao Cha kutegua kitendawili* kilichokuwepo ambapo *kikao hicho kimekuwa na Mafanikio makubwa.*
Miongoni mwa maazimio ya kikao hicho ni *Mkandarasi kukubali kuendelea na kazi* ambapo ameahidi kuwa ifikapo *January 31 mwakani Mradi utakuwa umekamilika na kukabidhiwa.*
Aidha *RC Makalla* amesema atafanya *ufuatiliaji wa fedha za Mkandarasi zipatikane kwa wakati* ili Hali hiyo isijirudie tena ambapo amemuelekeza *Katibu tawala wa Mkoa na Manispaa ya Kinondoni* kuhakikisha *wanashughulikia madai ya Mkandarasi.*
Hata hivyo *RC Makalla* amesema kupitia *meza ya maridhiano* Mkandarasi amekubali *kupunguza madai* alilokuwa akidai kutoka Shilingi *Milioni 664 hadi 265 sawa na 40%* ambapo amempongeza *Mkandarasi kwa kuonyesha uzalendo* huo.
Itakumbukwa kuwa *Agost 11* mwaka huu, Kitibu Mkuu wa CCM *Daniel Chongolo* alitembelea Mradi huo ambao ulianza *September 09/2019 na ulipangwa kukamilika September 13/ 2020* lakini Kutokana na changamoto za malipo Mradi huo haujakamilika adi Sasa Jambo lililomlazimu kutoa *maelekezo ya kupatiwa ufumbuzi.*



Post a Comment