RC MAKALLA AHIMIZA WANANCHI KUFANYA MAZOEZI

 










Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* ametoa msaada wa *Vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo Jezi, Mpira na Vifaa vya kufundishia* kwa Timu ya mpira wa Miguu ya *Masaki* akiwa Kama *Mlezi na kocha wa timu hiyo.*


Akizungumza wakati wa *Mazoezi* na Timu hiyo, *RC Makalla* amewahamasisha *Wananchi kufanya Mazoezi* ili kuimarisha Afya zao na kukabiliana na Magonjwa hususani *Corona.*


Aidha *RC Makalla* amesema akiwa kama Mlezi amedhamiria *kuipandisha Daraja timu ya Masaki na kuhakikisha inashiriki michuano* mbalimbali na ligi za ngazi ya juu ambapo kutakuwa na Timu ya *Masaki Vijana na Masaki Veterans.*


Pamoja na hayo, *RC Makalla* amesema August 14 ya Timu ya Masaki inatarajia *kushuka dimbani* kuikabili timu ya *Azam media* ambapo amejinasibu *kuigaragaza Timu ya Azam.*

0/Post a Comment/Comments