Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* leo August 10 ameshuhudia *awamu ya kwanza* ya utilianaji sahihi wa *mikataba 41 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 14.1* kwaajili ya Ujenzi wa Barabara za Mkoa wa Dar es salaam na kuwataka *Wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha Miradi kwa wakati na kwa kiwango.*
*RC Makalla* ametoa maelekezo hayo wakati wa *hafla ya utilianaji sahihi mikataba baina ya TARURA na Wakandarasi* ambapo amesema
mafanikio haya yote ni matokeo ya *kazi kubwa na nzuri* ya Serikali ya awamu ya sita Chini ya *Rais Samia Suluhu Hassan Katika utatuzi kero za Wananchi.*
Aidha *RC Makalla* amewaelekeza *DAWASA, TANROAD, TARURA, TTCL na TANESCO* kufanya kazi kwa pamoja ili kuondoa tatizo la *miradi kutomalizika kwa wakati* Kutokana na Taasisi husika *kuchelewa kuhamisha miundombinu.*
Pamoja na hayo *RC Makalla* amewaelekeza *TANROAD na TARURA* kuhakikisha wanasimamia *utunzaji wa miundombinu ya Barabara* ikiwa ni pamoja na *Usafi, ukarabati* na uwekaji wa *Vibao vya kuzuia biashara Kwenye eneo la hifadhi ya Barabara.*
Hata hivyo *RC Makalla* ameonyesha kufurahishwa na *ongezeko la bajeti ya Ujenzi wa Barabara Dar es salaam kutoka Shilingi bilioni 25 adi bilioni 40* na Nchi nzima kufikia *Bilion 300*.




Post a Comment