Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos
Makalla leo August 24 amezindua mfumo rasmi wa ukusanyaji wa malipo ya Ushuru
wa Maegesho kupitia njia ya Simu ambapo amesema Mfumo huo utakuwa suluhu ya
tatizo la Vishoka waliokuwa wakijipatia pesa ya Maegesho kwa njia ya
udanganyifu.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi
huo, RC Makalla amesema Mfumo huo utaanza rasmi kutumika Jijini humo September
mosi mwaka huu na utaenda kutatua kero na changamoto mbalimbali.
Miongoni mwa Changamoto ambazo RC
Makalla amesema zitakwenda kumalizwa na Mfumo huo ni Rushwa na mianya ya
Upotevu wa Mapato uliokuwa ukisababishwa na Ukusanyaji kwa njia ya Cash ambapo
mtu alikuwa na uwezo kufikisha Serikali kiasi kidogo Cha fedha kuliko kile
alichokusanya.*
Aidha RC Makalla amesema Mfumo huo
utatoa pia ufumbuzi wa kero ya uonevu na manyanyaso yaliyokuwa yakiwakuta Wenye
magari Kutokana na uwepo wa Watumishi wasiokuwa waadilifu.
Pamoja na hayo RC Makalla ameendelea kuwasisitiza TARURA na
Halmashauriza Dar es salaam kukamilisha utaratibu wa kuweka Vibao vya Wrong
Parking kwenye maeneo yote yasiyoruhusiwa kuegesha magari.
Mfumo wa Malipo ya Ushuru wa Maegesho kidigital unasimamiwa na TARURA na unamuwezesha Mwananchi kulipa kwa njia ya Simu ya mkononi au njia ya Bank ambapo baada ya kufanya malipo utapokea ujumbe ukikuonyesha kuwa malipo yamefika serikalini.

Post a Comment