.....................................
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla anatarajiwa kuanza rasmi ziara ya kusikiliza na kutatua kero na changamoto za Wananchi wa Mkoa huo Jimbo kwa Jimbo ikiwa ni Mpango wake wa kupatia ufumbuzi kero za Wananchi.
RC Makalla amesema ziara hiyo itaanza rasmi Jumatatu ya August 30kwenye Jimbo la Kawe Viwanja vya Tanganyika Packers, August 31 Jimbo la Kibamba, September 01Jimbo la Segerea, September 02 Jimbo la Mbagala na September 03 Jimbo la Kigamboni ambapo zoezi litaanza kuanzia Saa mbili Asubuhi Hadi majira ya jioni.
Aidha RC Makalla amesema kutakuwa na jopo la Wataalamu wabobeziwakiwemo Watendaji wa Serikali, Wanasheria, Kamishina wa Ardhi, Maafisa Ardhi, Jeshi la Polisi, TAKUKURU na Wadau wote wanaojihusisha na masuala ya kisheria.
Pamoja
na hayo RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi wote Wenye Migogoro kutumia Fursa
hiyo kuwasilisha Malalamiko yao ili yaweze kupatiwa ufumbuzi kwa mujibu wa
Sheria.


Post a Comment