Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu, akiwaeleza watanzania kupitia vyombo vya
habari kuwa Wizara yake imepokea kiasi cha shilingi bilioni 22.5 kutoka Hazina
kwa ajili ya kujenga vituo vya afya 90 kutokana na makusanyo ya tozo na
kusubiri nyongeza ya shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kujenga vituo vya afya
vingine 60 na kufanya idadi ya vituo hivyo vitakavyojengwa kufikia 150 katika
kipindi kifupi.
............................................................
SERIKALI imewaomba watanzania kuwa na subira wakati ikiendelea
kushughulikia suala la tozo ya miamala ya simu na kutoa taarifa ya makusanyo ya
fedha za tozo hizo katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita ambapo makusanyo
yalikuwa zaidi ya shilingi bilioni 48.4 ambazo zimepelekwa kwenye miradi ya
maendeleo katika sekta za afya, elimu na miundombinu ya barabara.
Akitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari jijini Dar es
Salaam, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwingulu Lameck Nchemba alisema kati
ya kiasi hicho cha fedha, shilingi bilioni 22.5 zimepelekwa TAMISEMI kwa ajili
ya ujenzi wa vituo vya afya 90, na kuahidi kupeleka kiasi kingine cha sh.
bilioni 15 mwezi Agosti, 2021 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vingine 60 na
kufanya idadi ya vituo vitakavyojengwa kufikia 150 nchi nzima.
Akifafanua kuhusu ujenzi wa vituo hivyo vya afya, Waziri wa
TAMISEMI, Mhe. Ummy Mwalimu alisema Wizara yake imepokea kiasi hicho cha
shilingi bilioni 22.5 na kiasi chote cha fedha kimepelekwa kwenye Halmashauri
husika na kiasi kingine cha sh. bilioni 15 zitakazotolewa mwezi Agosti ambapo
fedha hizo zote zitapelekwa katika Halmashauri 82 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo
vya Afya 150.
Pia Wizara ya TAMISEMI inatarijia kupokea sh. bilioni 12 kutoka
kwenye tozo, ambazo zitaenda kutumika kujenga vyumba vya madarasa 560 kwa ajili
ya shule za sekondari ili kukabiliana na uhaba wa madarasa kutokana na
sera ya elimu bila malipo, ambapo idadi ya wanafunzi inatarajia kuongezeka na
kufikia wanafunzi 944,855 ambao watahitaji madarasa 10,447.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-
Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil, alieleza kuwa kwa upande wa Zanzibar, katika
kipindi cha wiki nne tangu kuanza kutozwa kwa tozo za miamala ya simu, Serikali
imekusanya shilingi bilioni 1.6 ambazo zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo
Visiwani humo.
Naye Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, aliwahakikishia watanzania kuwa kikosi kazi kilichopewa majukumu ya kupitia upya gharama za tozo hizo kinaendelea kuchakata maagizo hayo na ndani ya mda mfupi watatoa mapitio yatakayotoa mwelekeo mpya katika hizo tozo na kuwaomba wa Tanzania kuendelea kuwa na subira na jambo hilO

Post a Comment